JIMBO la Bunda Mjini huenda
likaweka historia ya kuwa na idadi kubwa ya makada wa CCM waliojitokeza
kuchukua fomu za kuwania ubunge mkoani Mara, akiwamo mbunge wa zamani, Stephen
Wasira (pichani kushoto).
Hadi kufukia jioni jana
Jualai 15, 2020, jimbo hilo lilikuwa linaongoza kwa kuwa na makada wengi
waliochukua fomu za kuomba kuteuliwa na kugombea ubunge ukilinganisha na
majimbo mengine mkoani humo, kwa mijibu wa Katibu wa CCM Mkoa wa Mara, Shaibu
Ngatiche.
“Hadi jana (Jumatano) jimbo
lenye idadi kubwa ni Bunda Mjiini ambapo waliochukua fomu ya ubunge ni 60,” Ngatiche ameiambia Mara Online
News kwa njia ya simu leo asubuhi.
Ngatiche amesema jimbo la
Musoma Mjini lilikuwa linafuatia Bunda Mjini kwa kuwa na wananchama wa CCM
waliochukua fomu 54 likifuatiwa na jimbo la Serengeti (50).
Ametaja majimbo mengine na
idadi ya waliokuwa wamechukua fomu ya ubunge ikiwa kwenye mabano kuwa ni Rorya
(42), Bunda Vijijini (31), Musoma Vijijini (29), Tarime Vijijini (27) na Tarime
Mjini (18).
“Mkoa wetu unaweza kuwa na
idadi kubwa ya waliochukua fomu ya ubunge na tunategemea idadi hiyo kuongezeka
leo na kesho,” amesema katibu huyo wa CCM.
Shaibu Ngatiche |
Aidha, Ngatiche amesema wanachama
44 wa CCM wakiwemo vijana 12 wamejitokeza kuwania ubunge kupitia jumuiya mbalimbali
za chama hicho.
“Hadi sasa vijana kupitia
UVCCM wapo 12, Wazazi ni mmoja na kupitia UWT ni 31,” amesema Ngatiche.
Katika hali ya kuvutia,
maprofesa kadhaa wamejitokeza ‘kunyukana’ na mbunge wa Musoma Vijijini
anayemaliza muda wake, Profesa Sospeter Muhongo katika kinyang’anyiro cha
nafasi hiyo.
“Waliochukua fomu Musoma
Vijijini hadi kufikia jana (Jumatano) ni 29 wakiwemo maprofesa wengi,” amesema
Ngatiche.
(Imeandikwa na Mara Online News)
No comments:
Post a Comment