NEWS

Tuesday, 17 September 2024

Nyambari apokea kundi la wafanyabiashara maarufu kutoka India, wafanya ziara Zanzibar



Mfanyabiashara, mwandishi na mchapichaji wa vitabu maarufu Tanzania, Nyambari Nyangwine (mwenye kofia nyekundu) akiwa na kundi la wafanyabiashara maarufu kutoka nchini India katika ziara maalum kisiwani Unguja, Zanzibar mapema leo Septemba 17, 2024. Nyambari aliwapokea wafanyabiashara hao jana. (Na Mpigapicha Wetu)


Nyangwine ambaye amewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime mkoani Mara kwa tiketi ya chama tawala - CCM, amepokea wafanyabiashara hao ikiwa ni wiki chache zimepita baada ya kufanya ziara ya kibiashara ya wiki moja nchini India, ambapo pamoja na ratiba nyingine, alikutana na Waziri wa Utalii wa India, Shri Gajendra Singh Shekhawat na kumpatia zawadi ya bidhaa tofauti kutoka Tanzania, ikiwemo kahawa na majarida mbalimbali yanayoonesha vivutio vya utalii vilivyopo kwenye hifadhi za wanyamapori hapa Tanzania.

Baada ya India, Nyangwine alifanya ziara nyingine ya kibiashara ya siku saba katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ambako alitembelea miji mbalimbali na kukutana na watu tofauti katika nchi za Dubai, Abu Dhabi na Sharjah.

Wakifurahia jambo wakiwa kwenye usafiri


Mara baada ya kupokewa na
kukaribishwa na wenyeji wao Zanzibar
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages