NEWS

Tuesday, 17 September 2024

CSR Mgodi wa Barrick Bulyanhulu yawagusa watu wenye ulemavu Msalala



Baadhi ya watu wenye ulemavu waliopata baiskeli wakifurahia msaada huo uliotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu.
-------------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Msalala

Katika kutimiza wajibu wake kwa jamii, mgodi wa dhahabu wa Barrick Bulyanhulu uliopo wilayani Kahama, Shinyanga umegawa msaada wa vifaa mbalimbali kwa watu wenye ulemavu 53 ili kuwawezesha kujitegemea.

Vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi milioni 25, vilikabidhiwa kwa wahusika hao katika kata za Bulyanhulu na Bugarama zilizopo Halmashauri ya Msalala.

Mwakilishi wa Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Barrick Bulyanhulu, Lumbu Kambula alivitaja vifaa hivyo kuwa ni vyerehani, baiskeli, viti mwendo (wheelchairs), vifaa vya kusaidia usikivu, mashine za kuchomelea na vifaa saidizi kwa watu wenye ualbino.

Hafla ya makabidhiano ya vifaa hivyo, iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika ofisi za kata ya Bugarama, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa Uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii (CSR) wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu.

Mgodi huo umekubaliana na Halmashauri ya Msalala kwamba asilimia 10 ya fedha za CSR zitumike kusaidia makundi maalum, hasa wanawake, vijana, wazee na watu wenye ulemavu.

Afisa Tarafa ya Msalala, Victoria Lusana aliupongeza mgodi huo kwa kufanikisha kupatikana kwa vifaa wezeshi kwa wazee na watu wenye walemavu katika kata za Bugarama na Bulyanhulu, na kuwataka wanufaika kuvitumia na kuvitunza vifaa hivyo kwa malengo yaliyokusudiwa.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala, Judica Sumari alisema ushirikiano kati ya halmashauri hiyo na mgodi wa Bulyanhulu unalenga kuimarisha ustawi wa makundi mbalimbali ya jamii.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages