NEWS

Monday, 7 October 2024

Rais wa Barrick aongoza upandaji wa miti Shule ya Msingi mpya Kenyangi



Rais na CEO wa Barrick, Dkt Mark Bristow (kushoto) akipanda mti wa asili katika Shule ya Msingi mpya Kenyangi iliyojengwa na Mgodi wa Dhaha wa North Mara wakati wa kuikabidhi kijijini Matongo jana. Wa pili kulia ni Meneja Mkuu wa mgodi huo, Apolinary Lyambiko na baadhi ya wafanyakazi wake.
-------------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu/ Mara Online News

Rais na Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Barrick, Dkt Mark Bristow jana Jumapili aliongoza viongozi mbalimabali kupanda miti ya asili ambayo ni rafiki kwa mazingira katika Shule ya Msingi mpya Kenyangi katika kijiji cha Matongo wilayani Tarime, Mara.

Shule hiyo ambayo imegharimu mamilioni ya fedha imejengwa na Mgodi wa Dhahabu wa North Mara unaoendeshwa kwa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia Kampuni ya Twiga Minerals.

Dkt Mark akikata utepe wakati wa kukabidhi Shule ya Msingi mpya Kenyangi jana. (Picha zote na Mara Online News)
---------------------------------------------

Viongozi wengine waliopanda miti hiyo ni Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini, Mwita Waia, Meneka Mkuu wa Mgodi wa North Mara, Apolinary Lyambiko na Diwani wa Kata ya Matongo, Godfrey Kegoye.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages