Na Godfrey Marwa/ Mara Online News
Butiama
Butiama
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mara, Ibrahim Mjanakheri amewataka vijana kutokubali kutumiwa kuvuruga amani ya nchi kwa maslahi yao binafsi.
Pia, amewataka vijana kujiepusha na vitendo vya ushoga kwani ni kinyumbe cha maadili na mapenzi ya Mungu.
Mjanakheri akikagua ukakamavu wa vijana hao alipokwenda kufungua mafunzo yao.
------------------------------
Mjanakheri ameyasema hayo leo Oktoba 4, 2024 alipokwenda kufungua kambi la vijana 600 wanachama wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) kwa ajili ya mafunzo ya siku saba yanayofanyika kimkoa wilayani Butiama.
Lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwajenga vijana hao kimaadili na ukakamavu kwa ajili ya matembezi ya kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kutoka Butiama hadi Mwanza kushiriki kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka huu.
Amewataka vijana wanaoshiriki mafunzo hayo kuzingatia nidhamu wakati wote na baadaye kwenda kusemea mazuri yaliyofanywa na serikali.
"Vijana msishawishike na kauli za hao wanaotaka kuchafua amani ya nchi yetu, wakataeni na msiwakubalie. Tumieni makambi haya kwa lengo lililokusudiwa, na kikubwa ni kuzingatia nidhamu wakati wote wa mafunzo," amesisitiza Mjanakheri.
Aidha, Katibu huyo wa CCM amewakumbusha vijana kujitokeza kwa wingi kuomba nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
UNAWEZA PIA KUSOMA:
>>Jeshi la Polisi Tarime Rorya lazindua kampeni ya Tuwambie Kabla Hawajaharibiwa
>>Waziri Simbachawene azindua shule mpya iliyogharimu milioni 640/- Butiama, Sagini amshukuru Rais Samia
>>Naibu Rais Rigathi Gachagua aomba msamaha kwa Rais Ruto
>>Wanakijiji Serengeti 'wamwangukia' Waziri Simbachawene, aagiza wajengewe daraja
No comments:
Post a Comment