![]() |
Wabunge wakitoa maoni yao wakati wa kujadili hoja ya kumuondoa madarakani Gachagua |
-----------------------
Hatimaye bunge limefanya uamuzi wa kumuondoa naibu wa rais wa Kenya Rigathi Gachagua kupitia kura iliopigwa.
Katika kura hiyo, wabunge 281 waliunga mkono hoja ya kumuondoa kiongozi huyo madarakani huku wabunge 44 wakipiga kura kupinga na mmoja akikataa kupiga kura na hivyobasi kuafikia thuluthi mbili ya kura zilizohitajika ili kupitisha uamuzi wa kumuondoa afisini.
Gachagua anakabiliwa na msururu wa tuhuma zikiwemo ufisadi, kumhujumu rais na kuendeleza mgawanyiko wa kikabila.
Ni wabunge 233 pekee waliohitajika kuunga mkono hoja ya Gachagua kuondolewa.
“Ibara ya 145 (2) ya Katiba inaweka kizingiti cha angalau theluthi mbili ya wajumbe wa Bunge ili kuunga mkono hoja maalum ya pendekezo la kuondolewa kwa Naibu Rais wa Jamhuri ili hoja hiyo itekelezwe,” Spika Moses Wetang'ula alisema.
“Kwa mujibu wa matokeo ya uamuzi wa hoja niliyoitangaza hivi punde, jumla ya wajumbe 281 wakiwa ni zaidi ya theluthi mbili ya wajumbe wa Bunge hilo, wamepiga kura kuunga mkono hoja hiyo,” alisema.
"Bunge litaendelea na vikao vyake kesho Jumatano, Oktoba 9, 2024, ili kuendelea na shughuli za kawaida kama ilivyopangwa na Kamati ya Biashara ya Bunge."
Gachagua ndiye Naibu Rais wa kwanza kushtakiwa chini ya Katiba ya 2010.
Tarehe mosi mwezi Oktoba , 2024, Hoja Maalum ya kumwondoa Gachagua afisini kwa njia ya kushtakiwa iliwasilishwa na Mbunge wa Kibwezi Magharibi Mwengi Mutuse.
Mutuse aliwasilisha shutuma 11 dhidi ya Gachagua akimtuhumu kwa ufujaji wa pesa na kutumia wadhifa wake kutoa zabuni za serikali kwa kampuni zake miongoni mwa hoja zengine.
Chanzo:BBC
UNAWEZA PIA KUSOMA:
>>Makamu Mwenyekiti UVCCM Taifa azindua matembezi ya vijana kutoka Mara kwenda Mwanza
>>Mary Daniel afunga mafunzo ya vijana wa UVCCM Mara, ahimiza uzalendo kwa taifa
>>Rais wa Barrick akabidhi shule mpya ya kisasa iliyojengwa na mgodi wa North Mara
>>Jeshi la Polisi Tarime Rorya lazindua kampeni ya Tuwambie Kabla Hawajaharibiwa
No comments:
Post a Comment