NEWS

Thursday, 7 November 2024

DC Gowele ahimiza ubunifu vyanzo vya mapato Tarime Vijijini, watendaji wa kata wapewa pikipiki



Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Meja Edward Flowin Gowele akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Vijijini) kilichofanyika Nyamwaga jana Jumatano. (Picha na Godfrey Marwa)
------------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu/ Mara Online News

Mkuu wa Wilaya (DC) ya Tarime, Meja Edward Flowin Gowele ameihimiza Halmashauri ya Wilaya hiyo (Vijijini) kubuni vyanzo zaidi vya mapato na kuimarisha usimamizi wa matumizi yake.

Hata hivyo, akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo cha robo ya kwanza (Julai – Septemba) ya mwaka 2024/2025 kilichofanyika Nyamwaga jana Jumatano, Meja Gowele aliipongeza halmashauri hiyo kwa kusimamia vizuri ukusanyaji wa mapato.

Madiwani kikaoni

Wakati huo huo, halmashauri hiyo imekabidhi pikipiki tatu kwa maofisa watendaji wa kata za Regicheri, Kiore na Ganyange zilizotolewa na Serikali Kuu ili kurahisisha na kuboresha shughuli za kuhudumia wananchi.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Simion Kiles aliwataka watendaji hao kuzitunza na kuzitumia pikipiki hizo kwa malengo yaliyokusudiwa.

“Mzitunze vizuri, zifanye kazi zinazolengwa, mkifanya hivyo mtakuwa mnatusaidia sisi halmashauri kusaidia wananchi,” Kiles alisisitiza.

Makabidhiano ya pikipiki

Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages