Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Meja Edward Flowin Gowele akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Vijijini) kilichofanyika Nyamwaga jana Jumatano. (Picha na Godfrey Marwa)
------------------------------------------------
Mkuu wa Wilaya (DC) ya Tarime, Meja Edward Flowin Gowele ameihimiza Halmashauri ya Wilaya hiyo (Vijijini) kubuni vyanzo zaidi vya mapato na kuimarisha usimamizi wa matumizi yake.
Hata hivyo, akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo cha robo ya kwanza (Julai – Septemba) ya mwaka 2024/2025 kilichofanyika Nyamwaga jana Jumatano, Meja Gowele aliipongeza halmashauri hiyo kwa kusimamia vizuri ukusanyaji wa mapato.
Madiwani kikaoni
Wakati huo huo, halmashauri hiyo imekabidhi pikipiki tatu kwa maofisa watendaji wa kata za Regicheri, Kiore na Ganyange zilizotolewa na Serikali Kuu ili kurahisisha na kuboresha shughuli za kuhudumia wananchi.
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Simion Kiles aliwataka watendaji hao kuzitunza na kuzitumia pikipiki hizo kwa malengo yaliyokusudiwa.
“Mzitunze vizuri, zifanye kazi zinazolengwa, mkifanya hivyo mtakuwa mnatusaidia sisi halmashauri kusaidia wananchi,” Kiles alisisitiza.
Makabidhiano ya pikipiki
UNAWEZA PIA KUSOMA:
>>Mkurugenzi wa Kampuni ya Matari's Sales and Investment aipa Sekondari ya Bungurere msaada wa photocopy, kompyuta
>>Sekondari 11 Tarime Mji zanufaika na msaada wa vitabu kutoka Nyambari Nyangwine Foundation
>>MNEC Gachuma asimikwa kuwa Chifu wa Wakenye, Sekondari ya Manga yamtunuku cheti maalum
>>NECTA yatangaza matokeo ya darasa la saba 2024
No comments:
Post a Comment