Mwalimu Peter Sereka Marwa (mwenye suti nyeusi) akikabidhi msaada wa photocopy na kompyuta kwa Shule ya Sekondari Bungurere jana Novemba7, 2024.
--------------------------------------------
Mkurugenzi wa Kampuni ya Matari's Sales and Investment, Mwalimu Peter Sereka Marwa ameipatia Shule ya Sekondari Bungurere iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Vijijini) msaada wa mashine ya photocopy na kompyuta kwa ajili ya kudurufu mitihani ya wanafunzi.
Kwa mujibu wa Mwalimu Sereka, vifaa hivyo vina thamani ya shilingi zaidi ya milioni mbili.
"Vifaa hivi tumevitoa kwa kuwiwa bila mtazamo mwingine. Nimesoma katika shule hii, vifaa hivi vitumike kuboresha kiwango cha taaluma,” alisema Mwalimu Sereka wakati wa kukabidhi msaada huo shuleni hapo jana Novemba7, 2024.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Bungurere, Mwalimu Marwa Karera alimshukuru Mkurugenzi huyo kwa kujitolea kutoa msaada huo akisema ni watu wachache wanaokumbuka kurudi kusaidia shule walizosoma.
Nao wanafunzi wa shule hiyo, akiwemo Maria Wambura alishukuru na kuahidi kusoma kwa bidii baada ya changamoto ya vifaa hivyo kutatuliwa.
"Tumekuwa tukiandika mitihani ubaoni, kwa kuwa mmetupatia vifaa hivi, tutafanya vizuri kitaaluma," Maria alisema.
No comments:
Post a Comment