NEWS

Wednesday, 13 November 2024

Nyambari Nyangwine kuzuru Uganda kwa ziara ya kibiashara



Nyambari Nyangwine (kulia) na mmoja wa wasaidizi wake katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kabla ya 'kupaa' kuelekea nchini Uganda leo Novemba13, 2024.
----------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mfanyabishara, mwandishi na mchapishaji wa vitabu maarufu nchini, Nyambari Naywgine ameondoka leo Novemba 13, 2024 kuelekea jijini Kampala, Uganda kwa ziara ya siku tano ya kibishara.

Akizungumza na Mara Online News kwa njia ya simu muda mfupi kabla ya kuanza safari yake ya kwenda katika taifa hilo la Afrika Mashairiki, Nyambari amesema atapata fursa ya kutana na kampuni za uchapishaji, miongoni mwa mambo mengine.

Huo ni muendelezo wa ziara za kibiashara ambazo Nyambari anafanya katika mataifa ya ughaibuni.

Mfanyabiashara huyo amewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime, mkoani Mara kupitia chama tawala - CCM.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages