NEWS

Monday, 11 November 2024

Askari Uhifadhi auawa na tembo Tarime Vijijini



Tembo

Na Mwandishi Wetu/ Mara Online News

ASKARI Uhifadhi CR III - Arafat Saidi Miyimba (27) wa Hifadhi ya Taifa Serengeti, ameuawa na tembo katika kijiji cha Mrito wilayani Tarime, Mara, Kaskazini-Magharibi mwa hifadhi hiyo.

Arafat aliuawa Novemba 8, 2024 saa nne asubuhi, wakati akisaidiana na askari wenzake sita katika doria ya kuwafukuza tembo kutoka kijijini kuwarudisha hifadhini.

“Tembo walipokaribia kutoka vichakani walizungukwa na wananchi waliokuwa wakipiga yowe zilizosababisha tembo mmoja kurudi kuwakimbiza askari, ghafla Arafat alianguka akakanyagwa na mnyamapori huyo akafariki dunia papo hapo.

“Mwili wa CR III - Arafat umehifadhiwa katika Hospitali ya DDH Mugumu, wilayani Serengeti na utasafirishwa kesho [juzi] kwenda mkoani Morogoro kwa taratibu za mazishi,” ilieleza taarifa kwa umma iliyotolewa jana na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages