
Mshambuliaji wa Tabora United, Offen Chikola.
Na Mwandishi Wetu
Kamati ya Tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemchagua mshambuliaji wa Timu ya Tabora United, Offen Chikola kuwa mchezaji bora wa mwezi Novemba wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara msimu huu wa 2024/25.
Chikola ambaye aliisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa mechi tatu kati ya nne walizocheza na kufunga mabao matatu, yakiwemo mawili dhidi ya Yanga, amewabwaga wachezaji wenzake Yacouba Sogne na Moussa Camara wa Timu ya Simba.

Kocha Mkuu wa Azam, Rachid Taoussi.
Kwa upande mwingine, Kocha Mkuu wa Azam, Rachid Taoussi amechaguliwa kuwa kocha bora wa mwezi Novemba baada ya timu yake kushinda mechi zote tatu walizocheza mwezi huo, akiwashinda Fadlu David's wa Simba na Hamad Ali wa JKT Tanzania.
Aidha, Kamati ya Tuzo pia imemchagua Meneja wa Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma, Shaaban Rajabu kuwa Meneja Bora wa Uwanja kwa mwezi Novemba kutokana na usimamizi mzuri wa matukio ya kimichezo na kutunza miundombinu ya uwanja huo.
No comments:
Post a Comment