NEWS

Friday, 6 December 2024

Wabunge wa Tanzania wapata ajali wakienda mashindano ya michezo Kenya



Basi lililopata ajali

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Wabunge kadhaa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamejeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakitumia kusafiri kutoka Dodoma kwenda nchini Kenya kushiriki mashindano ya Michezo ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kugongana na lori la mizigo leo asubuhi eneo la Mbande mkoani Dodoma.

Taarifa zinasema majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa kutibiwa katika hospitali za Uhuru na Benjamini Mkapa za mkoani humo.

Basi lililopata ajali hiyo ni moja kati ya mabasi manne ya Shabiby yaliyokuwa yanasafirisha wabunge na watumishi wa Bunge zaidi ya 120 kwenda Mombasa, Kenya kushiriki mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza kesho Desemba7, 2024.

Tunaendelea na juhudi za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kuzungumzia tukio hilo.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages