NA MWANDISHI WETU, Arusha
----------------------------------------
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt Pindi Chana amesema maono na jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan za kutangaza vivutio vya utalii ndani na nje ya nchi,vimeifanya Tanzania iendelee kutwaa tuzo nyingi duniani na kujipatia heshima katika jumuiya ya kimataifa.
Amesema Rais Samia amekuwa mstari wa mbele katika kuboresha mazingira wezeshi ya biashara nchini, yakiwemo mageuzi makubwa katika sekta ya utalii.Waziri Chana aliyasema hayo jijini Dodoma jana alipowaongoza viongozi wakuu wa wizara yake kupokea Tuzo ya Kivutio Bora cha Utalii wa Safari Duniani 2024,wakati wa semina ya siku mbili inayoshirikisha maafisa wanyamapori wa wilaya nchini.
“Kwa Tanzania kutwaa Tuzo ya Kivutio Bora cha Utalii ni juhudi na maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuthamini na kutangaza sekta ya utalii kupitia filamu za “Tanzania The Royal Tour” na “Amazing Tanzania,” alisema.
Naye Naibu Waziri wa wizara hiyo, Dunstan Kitandula alisema tangu Rais Samia aingie madarakani amekuwa mstari wa mbele kukuza utalii kwa kushiriki kwenye filamu hizo, ambazo zimechangia ongezeko la watalii kufikia asilimia 96 kwa takwimu za Mei mwaka huu.
“Dkt Samia ameimarisha bajeti ya uendeshaji wa shughuli za uhifadhi na utangazaji utalii kwa kurejesha fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Utalii,” Kitandula alisema.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Maliasili, Benedict Wakulyamba alisema tuzo hiyo ni heshima kubwa kwa Tanzania kwani inakwenda kuwa chachu ya ongezeko la utalii nchini.
Wakulyamba aliahidi kuendelea kuboreshwa kwa mazingira wezeshi kwa watalii kwa kuongeza vivutio vipya.Hafla hiyo ya kupokea tuzo pia ilihudhuriwa na wenyeviti wa bodi na wakuu wa taasisi zilizo chini ya wizara, wakurugenzi/ wakuu wa vitengo na baadhi ya watumishi.

UNAWEZA PIA KUSOMA:
>>Hitilafu ya kiafya yambakisha Manula airport Simba ikipaa kwenda Algeria
>>MVIWANYA wakutanisha wadau kujadili maendeleo ya kilimo mseto
>>Ruto aahidi kuimarisha uchumi Afrika Mashariki
>>Barrick North Mara, Halmashauri ya Tarime wafikisha Kampeni ya Siku 16 ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia vijijini
No comments:
Post a Comment