
Aishi Manula
Na Mwandishi Wetu/ Mara Online News
Mlinda mlango wa timu ya Simba, Aishi Manula ameshindwa kuendelea na safari wakati timu hiyo ikielekea nchini Algeria leo kwa ajili ya mchezo wa pili wa makundi ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya timu ya Constantine ya Algeria, utakaochezwa Novemba 8, 2024, taarifa ya Simba imeeleza.
"Mlinda mlango Aishi Manula ameshindwa kuendelea na safari baada ya kupata hitilafu ya kiafya dakika chache kabla ya kuanza safari ya kuelekea nchini Algeria tukiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam," Klabu ya Simba imechapisha taarifa hiyo kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii.
Mwishoni mwa juma hili Simba na Yanga ambazo zinawakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa zitakuwa nchini Algeria ambapo kila moja itasaka alama tatu katika michuano ya Klabu Bingwa (Yanga) na Shirikisho (Simba) ili kuendelea na matumaini ya kusonga mbele katika mashinda hayo.
UNAWEZA PIA KUSOMA:
>>Jitihada za Rais Samia zajidhihirisha kwa ukuaji wa utalii nchini - Waziri
>>MVIWANYA wakutanisha wadau kujadili maendeleo ya kilimo mseto
>>Ruto aahidi kuimarisha uchumi Afrika Mashariki
>>Barrick North Mara, Halmashauri ya Tarime wafikisha Kampeni ya Siku 16 ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia vijijini
No comments:
Post a Comment