NEWS

Thursday, 5 December 2024

Mwenyekiti wa Mara Press ampongeza Soko kuchaguliwa kuongoza MISA - TAN



Mwenyekiti wa MRPC, Jacob Mugini. Picha ndogo ni Mwenyekiti mpya wa MISA - TAN, Edwin Soko.
-------------------------------------

Na Mwandishi Wetu/ Mara Online News

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara (MRPC), Jacob Mugini amempongeza Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza (MPC), Edwin Soko kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA – TAN), katika uchaguzi uliofanyika jana Desemba 4, 2024 jijini Dodoma.


Soko anachukua nafasi hiyo kutoka kwa Salome Kitomari aliyeiongoza MISA – TAN kwa kipindi cha miaka minane.

“Ninampongeza Soko kwa kuaminiwa na kuchaguliwa na wajumbe wa MISA – TAN kuwa Mwenyekiti wa Taasisi hiyo. Ninamhakikishia ushirikiano wa dhati kutoka kwa MRPC, na ninamtakia kila la heri katika utekelezaji wa majukumu yake mapya,” Mugini amesema katika mazungumzo na Mara Online News leo.

Mwenyekiti huyo wa MRPC amemwelezea Soko kama mtu mwenye upendo, anayepigania kwa dhati taaluma ya uandishi wa habari na uhuru wa vyombo vya habari.

“Nina matumaini makubwa kwamba chini ya uongozi wa Soko, MISA - TAN itakuwa na mafanikio makubwa na kuendelea kuwa sauti muhimu katika kulinda uhuru wa habari na kukuza taaluma ya habari Tanzania na Kusini mwa Afrika,” ameongeza Mugini ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari na Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Sauti ya Mara.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages