Waziri Dkt Dorothy Gwajima akizungumzia mikopo kwa wanawake na vijana wilayani Tarime Jumatatu iliyopita.
---------------------------------
Halmashauri mbili za wilaya ya Tarime zitavipatia vikundi vya wanawake na vijana mikopo ya shilingi takriban blioni 1.2 kutokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt Dorothy Gwajima alidokeza hilo Jumatatu iliyopita wakati akihutubia wananchi katika maadhimisho ya kilele cha kampeni ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia yaliyofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Ingwe, wilayani Tarime.
Alitaja halmashauri hizo na viwango vya mikopo ya fedha vitakavyotolewa vikiwa kwenye mabano kuwa ni Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (milioni 750) na Halmashauri ya Mji wa Tarime (shilingi milioni 450).
Waziri Gwajima aliziagiza halmashauri hizo kuanza kutoa mikopo hiyo wiki ijayo, vinginevyo zitakuwa matatani kama zitaichelewesha.
UNAWEZA PIA KUSOMA:
>>Lissu atangaza ‘vita’ ya kubadilisha uongozi wa juu CHADEMA
>>Barrick North Mara, Taifa Gas wagawa kanga doti 300 kwa wanawake kutoka vijiji jirani
>>Nyambari Nyangwine kuhudhuria uzinduzi wa filamu ya vivutio vya utalii nchini India kesho
>>Mgodi wa North Mara wawapa wanawake msaada wa majiko 222 ya gesi
No comments:
Post a Comment