
Na Mwandishi Wetu/ Mara Online News
Mgodi wa Dhahabu wa Barrick North Mara na Kampyni ya Taifa Gas wamegawa msaada wa kanga doti 300 kwa wanawake 246 kutoka vijiji 12 vinavyouzunguka, ikiwa ni sehemu ya kusherehekea kilele cha kampeni ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia.
Kanga hizo ambazo zilizotolewa jana, zimebeba ujumbe mahsusi wa kukemea ukatili wa kijinsia katika jamii.
Wanawake waliogawiwa kanga hizo watakuwa mabalozi wa kusambaza ujumbe huo na kampeni ya kupinga vitendo vya kupinga ukatili wa kijinsia ambavyo vimekuwa vikiathiri maendeleo ya wanawake.
Mgodi wa Barrick North Mara na Taifa Gas ni miongoni mwa wadau wakubwa waliofanikisha maadhimisho ya kilele cha Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia yaliyoofanyika kitaifa Nyamongo, wilayani Tarime Jumatatu iliyopita.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt Dorothy Gwajima.
Wakati wa maadhimisho hayo, mgodi wa North Mara kwa kushirikiana na Taifa Gas pia uligawa majiko 222 ya gesi kwa wanawake kutoka vijiji vinavyouzunguka ili kuwaondolea adha ya matumizi ya nishati ya kupikia isiyo salama.
No comments:
Post a Comment