NEWS

Monday, 10 February 2025

Hali za MNEC Gachuma, DC Kemirembe zaimarika, waruhusiwa hospitalini Bugando



Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Alfred Mtambi akimjulia hali MNEC Christopher Mwita Gachuma katika Hospitali ya Rufaa Bugando jana Jumatatu.
---------------------------------

Na Mwandishi Wetu

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayewakilisha mkoa wa Mara, MNEC Christopher Mwita Gachuma na Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Kemirembe Lwota ambao walipata ajali ya gari, wameruhusiwa kutoka hospitalini walikokuwa wakipata matibabu baadaya kupata ajali ya gari.

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Alfred Mtambi alithibitisha kuruhusiwa kwa viongozi hao katika Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza jana Jumatatu baada ya hali zao za kiafya kuimarika.

“Wote wawili wako stable (imara) na wameruhusiwa kutoka Hospitali, japo DC ataondoka usiku huu kwenda Dar es Salaam kwa uchunguzi zaidi, lakini yupo stable,” alisema RC Mtambi.
Kanali Mtambi akimjulia 
hali DC Kemirembe jana.
-------------------------------

MNEC Gachuma na DC Kemirembe walipata ajali ya gari eneo Rung’abure wilayani Serengeti juzi Jumapili wakati wakienda kumpokea Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa (Bara), Stephen Masato Wasira aliyekuwa akitokea wilayani Tarime katika mwendelezo wa ziara yake ya kikazi mkoani Mara.

Walipata maumivu na kusafirishwa kwa ndege kutoka Fort Ikoma, Serengeti kwenda Hospitali ya Rufaa Bugando kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa afya zao, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara.

Wasira akimjulia hali MNEC Gachuma jana
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages