MAKUMI ya abiria
wamejeruhiwa baada ya basi la Zakaria lililokuwa likitokea jijini Arusha
kuelekea wilayani Tarime, Mara kupata ajali ya kupinduka ndani ya Hifadhi ya
Taifa ya Serengeti.
Mhifadhi Mkuu wa hifadhi
hiyo, Misana Mwishawa, ameiambia Mara Online leo Ijumaa kwamba ajali hiyo
imetokea jana Aprili 23, 2020 katika eneo la Seronera.
Kwa mujibu wa Mwishawa, basi
hilo lilikuwa na abiria 43 na wahudumu watatu na kwamba waliojeruhiwa vibaya ni
dereva, kondakta na abiria mmoja wa basi hilo.
Massana Mwishawa mkuu wa hifadhi ya Serengeti
“Hao watatu waliojeruhiwa vibaya tulitumia gari letu dogo kuwapatia msaada wa kuwawahisha kwenda kupata matibabu wilayani Bunda kupitia lango letu la Ndabaka baada ya kushindwa kupita kwenye daraja la Grumeti wilayani Serengeti ambalo limefunikwa na maji.

“Majeruhi wengine
tumetumia madaktari wetu wa hifadhi kuwapatia matibabu ikiwa ni pamoja na
kushona majeraha bila malipo,” amesema Mwishawa.
Amesema abiria wengine
wote walipatiwa huduma za maji ya kunywa na malazi kwenye hosteli za hifadhi
bila malipo.
“Kwa sasa tunatafuta
chombo cha kunyanyua basi hili,” amasema Mhifadhi Mkuu huyo wa Hifadhi ya Taifa
ya Serengeti.
Tunaendelea na juhudi za
kumtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara kwa ajili ya kupata ufafanuzi zaidi
juu ya ajali hiyo.
(Habari na Christopher Gamaina)
No comments:
Post a Comment