NEWS

Sunday 17 May 2020

EWURA yazituza mamlaka kwa huduma bora za maji



MAMLAKA ya Uthibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Kaskazini imetoa tuzo na vyeti kwa Mamlaka ya Mji wa Moshi na Mamlaka ya Mji Mdogo wa Usa River kwa kufikia malengo ya kiutendaji ya utoaji huduma ya maji kwa wananchi kwa mwaka 2018/2019.

Akikabidhi tuzo hizo katika ofisi za EWURA jijini hapa juzi, Meneja wa Kanda hiyo, Mhandisi Lorivii Long'idu, amesema Moshi imeshika nafasi ya kwanza kitaifa, ikifuatiwa na Iringa na Mwanza.

Aidha, Mhandisi Long’idu amesema Usa River imekuwa ya kwanza kwa kuwasilisha kwa wakati tozo ya Ewura ya mwaka 2018/2019.

Amezipongeza mamlaka za maji Moshi na USA River kwa ushindi huo na kutaka uwe chachu ya kuboresha zaidi utendaji na utoaji wa huduma ya maji kwa wananchi

Kwa upande wake, Mwenyekti wa Mamlaka ya Maji Mji wa Moshi, Profesa Jafari Kideshesho, ameishukuru EWURA kwa kuona na kutambua huduma nzuri zinazotolewa na mamlaka hiyo.

Profesa Kideshesho ameahidi kuwa mamlaka hiyo itaendelea kutoa huduma bora ili pia iendelee kushika nafasi ya kwanza kitaifa mwaka ujao na kuendelea.

(Imeandikwa na Rose Jackson, Arusha)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages