Wakizungumza
na Mara Online News kwa nyakati tofauti jimboni humo hivi karibuni, wananchi
wamesema wanahitaji mbunge atayewasaidia kutatua kero mbalimbali zinazowakabili
na kuliweka jimbo hilo katika ramani ya maendeleo endelevu.
Diwani
mstaafu wa kata ya Kemambo, Agustino Sasi, amesema anatamani kuona jimbo hilo
likipata mbunge mpya mwenye utashi wa kulistawisha katika nyanja za kijamii na
kiuchumi.
“Tunahitaji
mbunge mpya mwneye uwezo wa kutatua matatizo yetu yaliyodumu kwa miaka mingi
sasa. Mfano, kuna tathmini iliyofanyika mwaka 2012 hapa Nyamongo kwa watu
wanaoishi jirani na mgodi wa North Mara, lakini mpaka leo hakuna
kilichotekelezwa. Tunataka mbunge atakayetatua hili,” amesema Sasi maarufu kwa
jina la Neto.
Ameongeza
kuwa angependa kuona safari hii anapatikana mbunge atayeunganisha wakazi wa
jimbo hilo na kuondoa mgawanyiko wa kikoo.
“Wabunge
waliopita wameshindwa kutetea hata mafao ya wazee wastaafu waboreshwe, wengi
tunalipwa kidogo sana na wengine hawalipwi kabisa.
“Ndio
maana safari hii tunataka mbunge anayefahamu matatizo ya wakazi wa jimbo la
Tarime Vijijini na mwenye uwezo wa kuyatafutia ufumbuzi wa kudumu,” amesisitiza
Sasi.
Hata
hivyo, Sasi ambaye ni mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), amesema anaridhishwa
na utendaji wa Rais Dkt John Magufuli akisema “Rais Magufuli anafanya kazi
nzuri sana.”
Esther
Masa kutoka kijiji cha Kegonga, amesema Tarime Vijijini inahitaji mbunge atakayejali
na kutetea maslahi ya wanyonge.
“Tunataka
mbunge atakayejali maisha ya watu wa chini, sio mbunge ambaye akichaguliwa anabadilisha
namba za simu,” amesema Masa na kuongeza:
Watalii wakitazama nyumbu wakivuka Mto Mara eneo la Kogatende |
Kwa
upande wake, Mwenyekiti mstaafu wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Amos Sagara,
amesema jimbo hilo linahitaji mbunge mwenye mtazamo mkubwa wa kimaendeleo bila
kujali chama cha siasa anachotaka.
Tarime inaongoza kuzalisha ndizi na kahawa aina ya Arabica Mkoani Mara |
Kutoka
kata ya Muriba, Washington Matiko amesema jimbo hilo linahitaji mbunge mzelendo
wa kweli na anayeshughulikia maendeleo ya wananchi kwa misingi ya usawa.
“Mbunge
tunayemhitaji awe ni ambaye pia ataona matatizo ya wakazi wa Tarime Vijijini kama
ni yake. Hatutaki mtu ambaye anatafuta ubunge kisha anatoweka jimboni,” amesema
Matiko.
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime wanaomaliza kipindi chao mwaka huu wakiwa kwenye kikao |
“Lakini
pia tunataka mbunge atakayeunganisha wananchi kuwa kitu kimoja na kutatua
migogoro ya kikoo,” amesisitiza Mkono.
Wananchi wa Tarime wakiwa katika mkutano uliofanyika jirani na mgodi wa North Mara kuzungumzia fidia |
Mwenyekiti
wa Kijiji cha Kerende, Muniko Magabe, amesema “Tunataka mbunge ambaye atakuwa
karibu na wananchi, sio mbunge wa kutengeneza migogoro katika jamii.”
Magabe
ameongeza “Kuna watu ambao sio wabunge lakini wanasaidia kutatua matatizo ya
wananchi. Watu kama hao wakipata ubunge wanaweza kupeleka maendeleo yetu mbali.”
Uchunguzi
uliofanywa na Mara Online News umebaini kuwa hadi sasa idadi ya wanasiasa
wanaomezea mate jimbo la Tarime Vijijini mwaka huu ni zaidi ya 20, huku wanaowania
jimbo la Tarime Mjini wakiwa zaidi ya 10.
Mbunge
wa Tarime Vijijini anayemaliza muda wake ni John Heche (Chadema).
(Habari na
Mwandishi Wetu, Tarime)
No comments:
Post a Comment