
Mwenyekiti Mara Press Club, Mugini Jacob (kushoto), akimpa pole Peter Zakaria kwa kuondokewa na kijana wake.
Tarime
-------------
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara (MRPC), Mugini Jacob, leo Machi 15, 2026 amefika nyumbani kwa mfanyabiashara maarufu Kanda ya Ziwa, Peter Zakaria ambaye pia ni Chifu wa Koo ya Watimbaru, kumpa pole kufuatia kifo cha kijana wake, Frank Peter Zakaria (41), kilichotokana na ajali ya gari Alhamisi wiki hii.
Jacob ametoa salamu za pole pia kwa niaba ya waandishi wa habari wa mkoa kwa Zakaria.

“Mzee wetu Peter Zakaria pole sana kwa msiba, tunamwomba Mungu awe mfariji mkubwa kwako, kwa mama na familia yako yote katika kipindi hiki kigumu,” Jacob ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mara Online na Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Sauti ya Mara amemwambia Peter Zakaria.
Mazishi ya Frank yanatarajiwa kufanyika kesho Jumatatu mjini Tarime nyumbani kwa mfanyabiashara huyo ambaye pia ni mmiliki wa mabasi ya Zakaria.

Pichani kwenye bango ni Frank Peter Zakaria enzi za uhai
No comments:
Post a Comment