Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda (kushoto) akisalimiana na mmoja wa watalii waliotembelea Hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Saanane. Mwenye fulana ya bluu nyuma yake ni Mkuu wa Hifadhi hiyo, Tutindaga George.
--------------------------------------------------
----------------------------------------
Furahia 88 Family & Derby Day imeweka historia ya pekee kwa kuwavutia watalii wa ndani, wakiwemo mashabiki wa timu za Simba SC na Yanga SC katika Hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Saanane iliyopo Ziwa Victoria jijini Mwanza.
Watalii wakiwemo mashabiki wa Simba na Yanga wakifurahia mandhari ya kuvutia ndani ya Hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Saanane.
------------------------------------------------
Awali, watani hao wa jadi walianza kufanya ziara ya kitalii na kujionea vivutio vya wanyamapori wa aina mbalimbali ndani ya Hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Saanane.
Ziara hiyo ilifunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda ambapo watalii 139 walijitokeza kufanya utalii na kutazama mtanange huo wa Simba na Yanga.
RC Mtanda akisalimia na wahifadhi.
-----------------------------------------------
Mtanda alituma wito kwa wakazi wa Mwanza kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo ndani ya mkoa huo, ikiwemo Hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Saanane.
Aidha, alilishauri Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kubuni vivutio vipya vya utalii ili kushawishi watalii wengi zaidi kupanga kutembelea hifadhi hiyo na jiji la Mwanza kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment