NA Mwandishi Wetu
-------------------------------
UWEPO wa madini mengi ya kimkakati mkoani Dodoma unalifanya eneo hilo la katikati ya Tanzania kuwa kitovu cha maendeleo kwa wananchi wake na taifa kwa ujumla.
Hiyo ni kauli ya Makamu wa Rais, Dkt Philip Mpango, alipopata fursa ya kutembelea mkoa huo na kukagua shughuli za maendeleo.
“Mwenyezi Mungu ametujaalia rasilimali hii ya madini ya kimkakati yenye mahitaji makubwa duniani. Ni lazima rasilimali hii itafsiriwe kwa maendeleo ya Dodoma na Tanzania kwa ujumla,” ameeleza Dkt Mpango wakati alipohitimisha ziara hiyo ya siku nne, Alhamisi, Agosti 22, 2024.
Alisema ili wananchi wa Tanzania waweze kufaidi matunda ya madini ya kimkakati yapatikanayo kwa wingi mkoani Dodoma, lazima Wizara ya Madini isimame kidete katika uvunaji wa madini hayo.
Katika historia ya maendeleo ya Tanzania, mkoa wa Dodoma umekuwa ukionekana kama ni eneo kame lisilostawi mazao mengi ya chakula. Lakini wataalam wa maendeleo wanasema mkoa huo ni tajiri siyo tu kwa zao la zabibu kama ilivyozoeleka kwa sasa, bali pia ni mkoa ulioficha hazina kubwa ya madini mengi, yakiwemo yale ya kimkakati yanayohitajika zaidi duniani.
Madini ya kimkakati Tanzania ni pamoja na kinywe, nikeli, kobati na mchanga mzito (lithium).
Haya ni madini yanayotumika katika teknolojia ya kisasa, ikiwemo ya utengenezaji wa betri za magari ya umeme na simu, oil, grisi, breki padi za magari, penseli na vizuia joto.
Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, akizungumza katika eneo la Mpwayungu wilayani Chamwino, wakati Makamu wa Rais akihitimisha ziara yake, alisema wizara inakamilisha andiko la mkakati wa usimamizi na uvunaji wa madini ya kimkakati ili kuchochea uchumi na kuendeleza sekta ya madini kwa ujumla.

No comments:
Post a Comment