Waziri wa Madini, Anthony Mavunde.
-------------------------------------------------
Na Mwandishi Wetu
Tanzania, nchi ambayo kwa sasa ina sera za kuwavutia wawekezaji katika sekta muhimu ya madini, imeeleza kuwa Mkutano wa Tano wa Kimataifa utakaofanyika Novemba 19 hadi 21, mwaka huu, utakuwa kivutio kwa wawekezaji duniani kote kuja kuwekeza vitega uchumi katika sekta hiyo.
Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, alieleza hayo jana jijini Dar es Salaam akisema mkutano huo utawavuta wawekezaji, watafiti, wachimbaji, wawakilishi wa serikali, viongozi wa mataifa ya kigeni na mabalozi wa nchi mbalimbali watakaokutana kujadili uongezaji thamani ya madini na uchimbaji wakati huu ambapo mahitaji ya madini yanaongezeka duniani.
Kaulimbiu ya mkutano huo itakuwa “Uongezaji Thamani Madini kwa Maendeleo ya Kijamii”, na utakuwa jukwaa muhimu la kutoa mwelekeo wa sekta ya madini nchini Tanzaia, kwa mujibu wa Waziri Mavunde.
Waziri huyo alisema mkutano huo utakuwa chachu ya fursa za uwekezaji kwa kuvutia kampuni za utafiti, uchimbaji, usindikaji madini.
Kusanyiko hilo la wadau wa madini duniani litatanguliwa na Onyesho la Vito litakalotangaza utajiri wa Tanzania katika sekta ya madini.
No comments:
Post a Comment