![]() |
Mgombea wa urais wa chama cha Democrat,Bi.Kamala Harris |
Kamala Harris amekubali rasmi uteuzi wake kama mgombea wa urais wa chama cha Democrat katika kongamano la kitaifa la chama hicho.
Mgombea huyo ameahidi kuongoza kwa ajili ya Wamarekani wote alipokuwa akitoa hotuba kuhusu uchaguzi kwa mamilioni ya Wademocrat iliyokamilisha kongamano la kitaifa la chama hicho.
Bi Harris amezungumzia masuala mbalimbali ya kitaifa ambapo kuhusu usalama wa mpaka, ambalo Republican wamekuwa wakitumia kumshambulia mgombea huyo wa Democratic.
Akizungumzia kuhusu mustakabal wa Marekani Bi Harris amesema:
"Ninaipenda nchi yetu kwa moyo wangu wote. Popote ninapoenda na kila mtu ninayekutana naye, naona taifa ambalo liko tayari kusonga mbele, tayari kwa hatua inayofuata na safari ya ajabu ya Marekani," anasema.
Amesema Wamarekani wana mengi zaidi sawa kuliko yale yanayowagawanya.
"Hakuna hata mmoja wetu anayepaswa kushindwa ili sisi sote tufanikiwe," anasema. Anatofautisha hili na kauli ya kampeni ya Trump, ambaye anasema " yuko huko akiidhalilisha Marekani".
Bi Harris pia amezungumzia kuhusu mswada wa usalama wa mpaka wa pande mbili ambao ulisambaratika katika Bunge la Congress mwaka huu baada ya Trump kuwataka Republican kupiga kura dhidi yake.
"Donald Trump anaamini kuwa makubaliano ya mpaka yataathiri kampeni yake, kwa hivyo aliamuru washirika wake katika Congress kuua mpango huo," Harris amesema.
"Sawa nakataa kucheza siasa na usalama wetu."
Harris anasema anapanga kurudisha mswada huo na kuutia saini kuwa sheria.
Idadi kubwa ya wahamiaji walizuiliwa kwenye mpaka wakati wa utawala wa Biden-Harris lakini idadi ya vivuko vya wahamiaji visivyo halali sasa imepungua kwa miezi mitano mfululizo.
Harris amesema kuwa nchi zinazoongozwa na watawala wa kimabavu "zinampigia debe Trump" kwa sababu wanaamini "ni rahisi kudhibiti kwa maneno ya kubembeleza na kupendelea".
"Wanajua Trump hatawajibisha watawala kwasababu anataka kuwa mbabe mwenyewe," aliuambia umati wa watu waliokuwa wakishangilia.

CHANZO:BBC
No comments:
Post a Comment