NEWS

Monday, 26 August 2024

Tume ya Uchaguzi: Wenye kadi za 2015, 2020 hawahusiki maboresho Daftari la Wapiga Kura




Na Mwandishi Wetu, Musoma

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania, Jaji (Mstaafu) Jacobs Mwambegele amesema uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura hauhusiani na kubadilika kwa jina la tume hiyo.

Hivyo, wananchi wenye kadi za kupiga kura zilizotolewa mwaka 2015 na 2020 hawahusiki na maboresho yajao ya daftari hilo ikiwa kadi zao hazijaharibika na kupotea.

Jina la Tume linalosomeka kwenye kadi zilizotolewa miaka hiyo ni “Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)” ambalo baada ya kubadilishwa sasa linasomeka “Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC).”

Jaji Mwambegele alitoa ufafanuzi huo katika mkutano wa tume hiyo na wadau wa uchaguzi mkoani Mara, uliofanyika mjini Musoma jana Agosti 25, 2024.

Sehemu ya wadau mkutanoni.
--------------------------------------

Jaji Mwambegele akizungumza.
-----------------------------------------

Katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo, Jaji Mwambegele alisema kufanikiwa kwa shughuli za uchaguzi kunatokana na ushiriki wa wadau.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uchaguzi - INEC, Ramadhani Kailima aliwasilisha mada kuhusu maandalizi ya maboresho ya Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, kabla ya mada ya mfumo wa maboresho hayo kuwasilishwa.

Maboresho ya daftari hilo yanatarajiwa kufanyika nchini kwa siku saba - kuanzia Septemba 4, mwaka huu, kwa mujibu wa mkurugenzi huyo.
Read Also Section

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages