NEWS

Sunday, 25 August 2024

Mara: Wanafunzi sita wafa Rorya wakiogelea bwawani




Na Mwandishi Wetu

Wanafunzi sita wa Shule ya Msingi ya Ochuna iliyopo wilaya ya Rorya Mkoani Mara walifariki dunia jana baada ya kuzama kwenye bwawa la mradi wa umwagiliaji wakati wakiogelea.

Taarifa kutoka eneo la tukio zimeeleza kwamba vifo vya wanafunzi hao vilitokana na kukwama kwenye tope ndani ya bwawa hilo la umwagiliaji.



Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Juma Chikoma amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba miili ya wanafunzi hao tayari imeshapatikana.

Habari za kuzama kwa wanafunzi hao zilitolewa na mwanafunzi mwenzao ambaye alibaki nje ya bwawa wakati wenzake wakiogelea. Read Also Section

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages