
Na Mwandishi Wetu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Salim Morcase amethibitisha kukamatwa kwa mmiliki wa gari lililosababisha vifo vya abiria wanane na wengine 20 kujeruhiwa wilayani Bunda.
Aidha, Kamanda Morcase ameviambia vyombo vya habari leo kwamba jeshi hilo linaendelea kumsaka dereva wa gari hilo aliyekimbia mara baada ya ajali hiyo.
Taarifa zinasema gari hilo lenye namba za usajili T 942 CZG lilimshinda dereva na kupinduka katika kijiji cha Nyandege wakati likitoka Mugumu wilayani Serengeti kuelekea Bunda jana.
No comments:
Post a Comment