DC Juma Issa Chikoka
-------------------------------
Na Mwandishi Wetu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na uhamisho wa viongozi mbalimbali, wakiwemo wakuu wa wilaya na wakurugenzi watendaji wa halmashauri.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt Moses Kasiluka na kusainiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais - Ikulu, Sharifa Nyanga, Rais Samia ameteua wakuu wa wilaya watatu na kuhamisha wengine 14.
Miongoni mwa hao ni Juma Issa Chikoka ambaye amehamishwa kutoka Rorya kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma, akichukua nafasi ya Dkt Khalfan Boniface Haule aliyehamishiwa Rorya mkoani Mara.
Naye Salum Hamis Abdallah Kali amehamishwa kutoka Kigoma kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Longido kuchukua nafasi ya Marko Henry Ng’umbi ambaye Rais Samia alitengua uteuzi wake juzi.
Wakuu wa wilaya wapya walioteuliwa na wilaya wanakopelekwa zikiwa kwenye mabano ni Luteni Kanali Fredrick Faustin Komba (Rufiji), Mohamed Mussa Mtulyakwaku (Uyui) na Olivanues Paul Thomas (Ludewa).
No comments:
Post a Comment