NEWS

Friday 20 September 2024

Wananchi wa vijiji 17 Musoma Vijijini washirikiana kujenga zahanati za vijiji vyao, serikali yatia mkono



Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini,
Profesa Sospeter Mwijarubi Muhongo.


Na Mwandishi Wetu/ Mara Online News

Wananchi wa vijiji 17 katika jimbo la Musoma Vijijini wameamua kushirikiana katika ujenzi wa zahanati za vijiji hivyo ili kuboresha huduma za afya.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi wa mbunge wa jimbo hilo juzi, tayari baadhi ya vijiji hivyo vimeanza kupokea michango ya ujenzi wa zahanati hizo kutoka serikalini.

Zahanati mpya zinajengwa katika vijiji vya Bulinga, Burungu, Butata, Chimati, Chirorwe, Kaburabura, Kakisheri, Kataryo, Kwikerege, Kurukerege, Kurwaki, Mabuimerafuru, Maneke, Nyabaengere, Nyambono na Nyasaungu

Jimbo la Musoma Vijijini linaongozwa na Prof Sospeter Mwijarubi Muhongo, linaundwa na kata 21 zenye vijiji 68.

Kwa sasa jimbo hilo lina Hospitali mpya ya Halmashauri ya Wilaya, vituo vya afya sita na zahanati 28, kati ya hizo, 24 ni za serikali na nne ni za binafsi.

“Wadau wa maendeleo, wakiwemo wazaliwa wa Musoma Vijijini, wanaombwa kuchangia ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya huduma za afya vijijini, ukiwemo ujenzi wa zahanati mpya,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo ya ofisi ya mbunge.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages