NEWS

Sunday 22 September 2024

Yanga yainyuka CBE 6-0, yatinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika



Nyota wa Yanga, Clement Mzize akimpangua kipa wa CBE na kumchapa bao kwenye uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar jana.
--------------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga SC imefanikiwa kufuzu hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Barani Afrika baada ya kupata ushindi mnono wa mabao 6-0 dhidi ya timu ya Benki ya Biashara ya Ethiopia CBE SA katika mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar jana usiku.

Mabao ya Yanga katika mchezi huo wa marudiano ya hatua ya 32 bora, yalifungwa na Mzambia Clatous Chama dakika ya 35, Clement Mzize dakika ya 46, Stephane Aziz Ki dakika ya 74 na 90 + 3, Mudathir Yahya dakika ya 88 pamoja na Duke Abuya dakika ya 90.

Kwa matokeo hayo, Yanga imefuzu hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika kwa ushindi wa jumla ya mabao 7- 0 kutokana na kuichapa CBE SA 1-0 kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Abebe Bikila jijini Addis Ababa, Ethiopia wiki iliyopita.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages