----------------
Na Mwandishi Wetu
Jeshi la Polisi, Mkoa wa Kipolisi wa Tarime-Rorya, mkoani Mara, leo limefanya zoezi la majaribio ya vitenda kazi vyake vya ulinzi ili kujiweka tayari kwa matukio ya aina yoyote ya uhalifu
Vitendea kazi hivyo – magari ya doria, magari ya maji washa, vikosi vya mbwa na farasi, usalama barabarani na kutuliza ghasia, vilionekana katika doria mitaa mbalimbali ya mji wa Tarime, Sirari na Rorya katika kuwaondoa hofu raia na kuwahakikishia ulinzi na usalama wao.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewana Jeshi hilo jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tarime–Rorya, SACP Mark Njera, amefanya ukaguzi wa vitendea kazi hivyo pamoja na ukakamavu wa askari kuhakikisha wepesi wao katika kukabiliana na matukio ya uhalifu.
Amewapongeza askari hao kwa utimamu wao uliotokana na mazoezi ya mara kwa mara.

No comments:
Post a Comment