NEWS

Sunday, 6 October 2024

Naibu Rais Rigathi Gachagua aomba msamaha kwa Rais Ruto

Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua(kushoto) na Rais William Ruto
 ------------------------------
Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua, ambaye anakabiliwa na hatari kuondolewa madarakani, amemuomba msamaha mkuu wake, Rais William Ruto.

Bw Gachagua alitoa ombi hilo kwa Ruto mapema  Jumapili, Oktoba 6, akisema kwamba ingawa hajui kosa lolote, anataka apewe nafasi nyingine ya kuwahudumia Wakenya.

“Nataka kumuomba ndugu yangu, Rais William Ruto: ikiwa nimekukosea kwa namna yoyote katika jitihada zetu za kufanya kazi, tafadhali fungua moyo wako na unisamehe,” Bw Gachagua ameyasema hayo akiwa kanisani huko Karen, jijini Nairobi.

Maombi ya Righathi kwa Rais Ruto hayakuishia kwake tu, "Ikiwa mke wangu (Dorcas Rigathi) amekukosea kwa njia yoyote tafadhali fungua moyo wako kumsamehe."

Naibu Rais huyo aliyekalia kuti kavu amewaomba msamaha wabunge, na pia rai awa kawaida wa msamaha pia kama huo kwa Wakenya waliotaka aondolewe madarakani wakati wa ushiriki wa umma katika kutoa maoni.

"Kwa watu wa Kenya, katika utumishi wetu kote nchini, tunapokuhudumia, ikiwa kuna jambo lolote ambalo tumefanya au kusema ambalo unaona halifai, ambalo unaona halikubaliki, tafadhali unisamehe."

Hali ya kisiasa imepamba moto nchini Kenya toka mwanzoni mwa juma lililopita baada ya hoja ya kutaka kumuondosha madarakani Bw Gachagua ilipowasilishwa rasmi bungeni na kupokelewa.

Hivi sasa michakato ya kikatiba inaendelea katika kufanikisha ama kuiangusha hoja hiyo.

Wandani wa Rais wa Kenya William Ruto waliwasilisha hoja bungeni siku ya Jumanne ya kumshtaki Naibu Rais Rigathi Gachagua wakimtuhumu kwa kuchochea chuki za kikabila na kuidhoofisha serikali.

Pia wanadai kwamba Gachagua amejihusisha na masuala ya ufisadi , kuihujumu serikali na kukuza siasa za kikabila. Tofauti kati ya rais Ruto na Gachagua zimeongezeka katika siku za hivi karibuni.

Gachagua anasema ametengwa na amekanusha shutuma za washirika wa Ruto kwamba alihusika na maandamano ya kupinga serikali mapema mwaka huu. 
Chanzo:BBC
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages