Mwenyekiti wa Mara Regional Press Club, Jacob Mugini (kushoto) akimkabidhi Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa North Mara, Apolinary Lyambiko cheti cha pongezi kutambua mchango muhimu wa mgodi huo katika kukuza uchumi wa mkoa wa Mara. Kulia ni Meneja Mahusiano wa mgodi huo, Francis Uhadi.
---------------------------------------------
Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara (MRPC) imeutunuku Mgodi wa Dhahabu wa North Mara cheti cha pongezi kuonesha kutambua mchango wake katika kukuza uchumi wa mkoa huo.
Mwenyekiti wa MRPC, Jacob Mugini alikabidhi cheti hicho maalum kwa Meneja Mkuu wa mgodi huo, Apolinary Lyambiko wakati wa ziara ya wanachama wa klabu hiyo mgodini hapo jana.
GM Lyambiko akizungumza na waandishi hao.
--------------------------------------------
Katika ziara hiyo ya siku moja, waandishi hao walielezwa maendeleo ya shughuli za mgodi huo na kujionea baadhi ya miradi ya huduma za kijamii uliyoitekeleza katika vijiji vinavyouzunguka.
Walitembelea Shule ye Msingi mpya Kenyangi iliyojengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 1.287 na mradi wa kilimo biashara unaoendeshwa na vijana katika kijiji cha Matongo.
Picha zote na Mara Online News
-------------------------------------------
Mgodi wa North Mara kupitia mpango wake wa Uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii (CSR), hutenga mabilioni ya fedha kila mwaka kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kijamii katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime.
Mgodi huo unaendeshwa na Kampuni ya Barrick kwa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia Kampuni ya Twiga Minerals.
No comments:
Post a Comment