Mwanariadha wa Kenya Ruth Chepngetich amevunja rekodi ya dunia kwa kushinda mbio za masafa marefu za Chicago Marathon Jumapili.
Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 30 alitumia muda wa saa mbili, dakika tisa na sekunde 57 na hivyo kupita rekodi ya awali ya Tigst Assefa wa Ethiopia kwa karibu dakika mbili.
Chepngetich ndiye mwanamke wa kwanza kukimbia marathon chini ya saa mbili na dakika 10.

Assefa aliweka rekodi ya awali kwa ushindi wa Berlin Marathon 2023 kwa saa mbili, dakika 11 na sekunde 53.
"Ninajisikia vizuri sana, ninajivunia. Hii ni ndoto yangu ambayo imetimia," alisema Chepngetich, bingwa wa dunia wa marathon 2019.
"Nimepigana sana nikifikiria rekodi ya dunia na nimeitimiza."
Ushindi kwa Chepngetich ni wa tatu kwake huko Chicago, ambapo alishindwa kuvunja rekodi ya dunia ya wakati huo ya Brigid Kosgei kwa sekunde 14 mnamo 2022 .
Mashindano manne ya mbio za Marathon kati ya matano ya kasi zaidi ya wanawake yamekuwa yakifanyika Chicago katika kipindi cha miaka sita iliyopita.
Chanzo:BBC
No comments:
Post a Comment