NEWS

Friday, 11 October 2024

RC Mtambi azindua uandikishaji wapiga kura Mara



Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi (kushoto) akijiandikisha kwenye kituo cha wapiga kura Mkendo mjini Musoma leo Oktoba 11, 2024 kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
--------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu/ Mara Online News
Musoma

Mkuu wa Mkoa (RC) wa Mara, Kanali Evans Mtambi amezindua uandikishaji wa wapiga kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika mkoa huo.

RC Mtambi amezindua uandikishaji huo mapema leo asubuhi Oktoba 11, 2024 kwa kujiandikisha katika kituo cha ofisi za kata ya Mkendo iliyopo Manispaa ya Musoma.

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utafanyika nchini kote Novemba 27, 2024 ukiwa na kaulimbiu inayosema “Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze Kushiriki Uchaguzi.”
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages