NEWS

Wednesday, 20 November 2024

Uchaguzi Serikali za Mitaa: Lissu kuzindua kampeni za CHADEMA Kanda ya Serengeti



Tundu Lissu

Na Mwandishi Wetu/ Mara Online News

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tanzania Bara, Tundu Lissu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kampeni za chama hicho - za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, utakaofanyika mjini Tarime, mkoani Mara kesho Novemba 21, 2024.

Hiyo ni kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na ofisi za CHADEMA Wilaya ya Tarime na Kanda ya Serengeti inayoundwa na mikoa ya Mara, Simiyu na Shinyanga.

Kampeni za uchaguzi wa viongozi wa Serikali za Mitaa zinatarajiwa kuhitimishwa Novemba 26 ili kupisha uchaguzi wenyewe uliopangwa kufanyika nchini kote Novemba 27, 2024.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages