NEWS

Monday, 18 November 2024

Mfanyabiashara wa Tanzania Nyambari Nyangwine sasa kuwekeza Uganda



Nyambari Nyangwine (wa pili kutoka kulia) akiwa nchini Uganda.

Na Mwandishi Maalumu

Mfanyabiashara wa Tanzania, Nyambari Nyangwine ametangaza kuwekeza katika taifa jirani la Uganda.

Nyangwine ambaye ni mwandishi na mchapishaji maarufu wa vitabu nchini, alitangaza uamuzi huo jana Jumapili mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku tano ya kibiashara katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

“Ziara yangu imekuwa ya mafanikio na nitafungua ofisini Uganda immediately (haraka),” Nyambari aliliambia Gazeti la Sauti ya Mara kutoka Uwanja wa Kimataifa wa Entebbe, Uganda akiwa tayari kurejea Tanzania.

Alisema ofisisi hiyo itakuwa ikijishugulisha na uandishi, uchapishaji, uuzaji na usambazaji wa vitabu nchini Uganda.

Nyambari Nyangwine (wa nne kutoka kushoto) akiwa nchini Uganda.

Akiwa Uganda, Nyambari alikutana na wataalamu wa elimu, waandishi, wachapaji na wauzaji wa vitabu na magari.

“Mipango yetu ni kufungua ofisi nchini Uganda Desemba mwaka huu, nimeacha wasaidizi wangu wakiendelea na taratibu na maandalizi yote muhimu,” alisisitiza mfanyabiashara huyo wa Tanzania na kada wa chama tawala - CCM ambaye amewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime, mkoani Mara.

Nyambari ambaye ni Mwenyekiti wa Nyambari Nyangwine Group of Companies, pia ameanzisha Taasisi ya Nyambari Nyangwine (NNF) kuunga mkono juhudi za serikali katika uboreshaji wa huduma za elimu na afya nchini.

Pia, kutengeneza ajira kwa vijana kupitia uboreshaji ya elimu ya ujasiriamali na kukukuza utamaduni wa Mtanzania kikanda na kimataifa, huku suala la lugha ya Kiswahili likipewa kipaumbele.

Taasisi hiyo ilizinduliwa jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mwanaidi Ally Khamis kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages