
Wapiga kura wa Marekani watachagua, kati ya Makamu wa Rais wa chama cha Democratic, Kamala Harris na Donald Trump wa Republican.
Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya uchaguzi mkuu nchini Marekani, ni wakati wa kuzielewa sera za wawili hao.
Mfumuko wa bei
Harris anasema kipaumbele chake kitakuwa ni kupunguza gharama ya bei ya chakula na nyumba kwa familia.Ameahidi kupiga marufuku kupandisha bei bidhaa za vyakula na matumizi ya nyumbani, kuwasaidia wanaonunua nyumba kwa mara ya kwanza na kuongeza upatikanaji wa nyumba
Mfumuko wa bei uliongezeka chini ya urais wa Biden, kama ilivyokuwa katika nchi nyingi za magharibi, baada ya Covid na vita vya Ukraine.
Trump ameahidi "kukomesha mfumuko wa bei na kuifanya Marekani iweze kuishika tena."
Ameahidi kutoa viwango vya chini vya riba, (ingawa jambo hilo haliko chini ya udhibiti wa rais,) na kuwafukuza wahamiaji wasio na vibali akiamini kutapunguza mzigo kwa makazi.Wanauchumi wanaonya ahadi yake ya kutoza ushuru wa juu zaidi kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje inaweza kuongeza bei.
Kodi
Harris anataka kuongeza ushuru kwa biashara kubwa na kwa Wamarekani wanaingiza dola za kimarekani 400,000 (£305,000) kwa mwaka.
Pia ameahidi hatua kadhaa ambazo zitapunguza mzigo wa ushuru kwa familia, ikiwa ni pamoja na kuongeza malipo kwa familia zenye watoto.
Pia atapunguza ushuru wa faida kwa mauzo ya vitu, iwe wastani wa 23.6% hadi 28% ikilinganishwa na 44.6% ya Joe Biden.
Trump anapendekeza kupunguza ushuru, ikiwa ni pamoja na kuendeleza punguzo kama lile la 2017 – ambalo zaidi liliwanufaisha matajiri.
Utoaji mimba
Harris ameifanya haki za uavyaji mimba kuwa sehemu muhimu katika kampeni yake, na anaendelea kutetea sheria ambayo itazingatia haki za kutoa mimba nchini kote.
Trump hana sera inayoeleweka kuhusu uavyaji mimba.
Majaji watatu aliowateua katika Mahakama ya Juu wakati akiwa rais walihusika katika kubatilisha haki ya kikatiba ya kutoa mimba nchini kote, na uamuzi ukaachwa kwa majimbo.
Uhamiaji
Harris alipewa jukumu la kushughulikia mgogoro wa uhamiaji huko kusini na kukusanya mabilioni ya dola, pesa binafsi ili kufanya uwekezaji wa kikanda.
Watu waliovuka mpaka kutoka Mexico mwishoni mwa 2023 ilikuwa kubwa lakini idadi imepungua tangu kwa sasa. Katika kampeni hii, amerudia msimamo wake na kusisitiza ana uzoefu kama mwendesha mashtaka huko California katika kukabiliana na walanguzi wa binadamu.
Trump ameapa kufunga mpaka kwa kukamilisha ujenzi wa ukuta na kuongeza ulinzi. Pia ameahidi kuwahamisha kwa makundi wahamiaji wasio na vibali.
Wataalamu waliiambia BBC jambo hilo linaweza kukabiliwa na changamoto za kisheria.
Sera za kigeni
Harris ameahidi kuunga mkono Ukraine. Ameahidi, ikiwa atachaguliwa, atahakikisha Marekani na sio China, ndio inashinda "ushindani wa Karne ya 21."
Amekuwa mtetezi wa muda mrefu wa suluhisho la serikali mbili kati ya Waisraeli na Wapalestina, na ametoa wito wa kusitishwa vita huko Gaza.
Trump ana sera ya kigeni ya kujitenga na anataka Marekani ijitenge na migogoro ya maeneo mengine duniani.
Amesema atamaliza vita nchini Ukraine ndani ya saa 24 kupitia maafikiano na Urusi. Trump amejiweka kama mfuasi mkuu wa Israel lakini hajasema kuhusu jinsi atakavyomaliza vita huko Gaza.
Biashara
Harris amekosoa mpango wa Trump wa kutoza ushuru bidhaa zinazotoka nje, akiuita ushuru huo utaigharimu kila kaya dola 4,000 kwa mwaka.
Anatarajiwa kuwa na sera za kulenga kutoza ushuru baadhi tu kutoka nje, na atadumisha ushuru ambao utawala wa Biden-Harris uliuanzisha, kama ule wa uagizaji wa magari ya umeme kutoka China.
Kwa Trump, ushuru ni ahadi yake kuu katika kampeni hii. Amependekeza ushuru mpya wa 10-20% kwa bidhaa nyingi za kigeni, na ushuru mkubwa zaidi kwa zile zinazotoka China.
Pia ameahidi kuyashawishi makampuni kuweka makazi yao Marekani ili kutengeneza bidhaa, kwa kuwapa kiwango cha chini cha ushuru.
Mabadiliko ya Tabia nchi
Harris, kama makamu wa rais, alisaidia kupitisha Sheria ya Kupunguza Mfumuko wa Bei, ambayo itatumia mabilioni ya dola katika nishati mbadala, na punguzo la kodi ya magari ya umeme.
Lakini ameacha kupinga upasuaji wa miamba kwa ajili ya kupata gesi na mafuta, mbinu inayopigwa na wanamazingira.
Trump, akiwa katika Ikulu ya White House, aliondoa mamia ya kanuni za ulinzi wa mazingira, ikiwa ni pamoja na vikwazo vya utoaji wa hewa chafu kutoka katika mitambo na magari.
Katika kampeni hii ameapa kupanua uchimbaji wa mafuta huko Arctic na kushambulia magari ya umeme.
Huduma ya afya
Harris, amekuwa sehemu ya utawala wa White House ambao umepunguza gharama za dawa na kupunguza bei ya insulini kwa dola 35.
Trump, mara nyingi ameapa kuivunja Sheria ya Huduma ya bei nafuu, amesema akichaguliwa ataiboresha tu, bila kutoa maelezo ni vipi. Sheria hiyo imekuwa muhimu katika kupata bima ya afya kwa mamilioni ya watu.
Anataka matibabu ya uzazi yanayofadhiliwa na walipa kodi, lakini hilo linaweza kupingwa na Republicans katika Congress.
Sheria na uhalifu
Harris ameelezea uzoefu wake kama mwendesha mashtaka na kumtaja Trump kuwa amepatikana na hatia ya uhalifu.
Trump ameapa kuharibu mashirika ya dawa za kulevya, kuangamiza ghasia za magenge na kujenga upya miji inayoongozwa na chama cha Democratic ambayo anasema imejaa uhalifu.
Amesema atatumia jeshi au kikosi cha akiba, kukabiliana na wapinzani anaowaita "maadui wa ndani" na "wendawazimu wa mrengo wa kushoto" ikiwa watavuruga uchaguzi.
Bunduki
Harris ameahidi kuzuia vurugu za bunduki, licha ya kuwa yeye na Tim Walz - wote wanamiliki bunduki – lakini wanatetea sheria kali za umiliki. Lakini hatua za kupanua ukaguzi au kupiga marufuku silaha kubwa zitahitaji msaada wa Congress.
Trump amejiweka kama mtetezi wa wamiliki bunduki, haki ya kikatiba ya kubeba silaha. Akihutubia Chama cha Kitaifa cha Wamiliki Bunduki mwezi Mei, alisema ni rafiki yao mkubwa.
Bangi
Harris ametoa wito wa kuharamishwa bangi kwa matumizi ya burudani. Anasema watu wengi wamepelekwa gerezani kwa kumiliki na kusema idadi kubwa ya wanaokamatwa ni wanaume weusi na Walatino.
Trump amelegeza msimamo wake na kusema ni wakati wa kukomesha "kukamatwa bila sababu na kuwafungwa" watu wazima kwa kuwa na kiasi kidogo cha bangi kwa matumizi binafsi.
Chanzo:BBC
UNAWEZA PIA KUSOMA:
>>Nyambari Nyangwine Foundation yagawa msaada wa vitabu kwenye sekondari za Halmashauri ya Tarime Mji, wanafunzi waahidi matokeo mazuri
>>Rais Samia ataja mambo yatakayowezesha Tanzania kuwa ghala la chakula barani Afrika
>>NECTA yatangaza matokeo ya darasa la saba 2024
>>MAKALA MAALUMU:Ajenda ya nishati safi ya kupikia na ugumu wa biashara ya mkaa mjini Bukoba
No comments:
Post a Comment