NEWS

Tuesday, 10 December 2024

Coastal Union waachana na kipa wao Ley Matampi



Ley Matampi

Na Mwandishi Wetu

Timu ya Coastal Union ya Tanga imetangaza kuachana na aliyekuwa mlinda lango wake, Ley Matampi, 35, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kwa makubaliano ya pande zote mbili.

"Tumefikia makubaliano baina ya klabu yetu na golikipa wetu Ley Matampi ya kumaliza huduma za pande zote mbili, uzoefu wako umechangia kwa asilimia kubwa mafanikio yetu ya msimu uliopota", taarifa ya Coastal imeeleza.

Mlinda mlango huyo wa zamani wa TP Mazembe alijiunga na Coastal Union msimu uliopita na kucheza kwa mafanikio makubwa mpaka kuibuka golikipa bora wa msimu wa 2023/24 wa Ligi Luu ya NBC katika tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages