
Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa anayewakilisha Mkoa wa Mara, Dkt Paul Thomas Mwikwabe, akikabidhi msaada wa majiko ya gesi kwa mama lishe wakati wa ziara yake Musoma Vijijini jana Desemba 10, 2024.
-------------------------------------
Mjumbe wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa anayewakilisha Mkoa wa Mara, Dkt Paul Thomas Mwikwabe, amefanya ziara katika Halmashauri ya Musoma Vijijini na kuwahamasisha mama lishe kutumia nishati ya kupikia kwa kuwapa baadhi yao majiko ya gesi.

Dkt Mwikwabe alitoa msaada huo wa majiko jana kuunga juhudi za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kumtua mama kuni kichwani na kumuepushia adha ya matumizi ya nishati ya kupikia isiyo salama.
Pia, aliwapa wajasiriamali hao msaada wa mavazi maalumu kwa shughuli zao katika eneo la Murangi.

Kwa upande mwingine, Dkt Mwikwabe alikutana na kuzungumza na waendesha ‘bodaboda’ eneo la Suguti na kuwapa baadhi yao msaada wa vizibao (reflectors).

Mjumbe huyo wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa yuko katika ziara ya siku nne ya kuhamasisha uhai wa jumuiya hiyo katika wilaya za mkoa wa Mara.
Anatumia fursa hiyo pia kuwapongeza na kuwashukuru vijana kwa kushiriki na kukipatia chama tawala - CCM ushindi mkubwa katika uchaguzi wa viongozi wa Serikali za Mitaa uliofanyika nchini kote Novemba 27, 2024.
Sambamba na hayo, Dkt Mwikwabe anasisitiza umuhimu wa vijana kuweka mipango mikakati ya kuhakikisha chama hicho kinaendelea kushinda katika chaguzi na kuchochea maendeleo ya mkoa wa Mara na taifa kwa ujumla.
UNAWEZA PIA KUSOMA:
>>Mgodi wa North Mara wawapa wanawake msaada wa majiko 222 ya gesi
>>HABARI PICHA:Waandishi wa habari Mara kushiriki kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia
>>Rais wa Syria adaiwa kuikimbia nchi, waasi wafungulia wafungwa gerezani
>>Wabunge wa Tanzania wapata ajali wakienda mashindano ya michezo Kenya
No comments:
Post a Comment