
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Patrick Chandi Marwa.
--------------------------------
Na Mwandishi Wetu/ Mara Online News
Serikali imeupatia mkoa wa Mara shilingi trilioni 1.2 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ili kaharakisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika mkoa huo.
Taarifa kwa umma iliyotolewa Jumamosi iliyopita na CCM Mkoa wa Mara baada ya kikao cha kawaida cha Halmashauri Kuu ya Chama Mkoa kilichoongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Patrick Chandi Marwa, ilisema fedha hizo zimetolewa katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Hata hivyo, taarifa hiyo haikutaja aina ya miradi iliyotekelezwa hadi sasa na ambayo utekelezaji wake unaendelea.
Kwa upande mwingine, taarifa hiyo ilisema kikao hicho cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Mara kimewapongeza na kuwashukuru wanachama na wananchi wa mkoa huo kwa kukipatia chama hicho ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa viongozi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Novemba 27, mwaka huu.
“Aidha, kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Mara kimemshukuru sana Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuleta kiasi cha shilingi trilioni 1.2 za miradi ya maendeleo,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
UNAWEZA PIA KUSOMA:
>>TAMISEMI yatangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza 2025
>>Dkt Machage atembelea ofisi za Gazeti la Sauti ya Mara, alipongeza kwa kazi nzuri
>>Mama Samia Legal Aid yafikisha msaada wa kisheria bila malipo kwa wananchi mkoani Mara
>>Rorya:Diwani ajitolea kuwalipa mshahara wenyeviti wa vitongoji 26 katani Rabuor, ni GSN Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya
No comments:
Post a Comment