NEWS

Monday, 16 December 2024

Rorya: Diwani ajitolea kuwalipa mshahara wenyeviti wa vitongoji 26 katani Rabuor, ni GSN Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya



Diwani wa Kata ya Rabour na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, Gerald Ng'ong'a.
------------------------------------

Na Mwandishi Wetu/ Mara Online News

Diwani wa Kata ya Rabuor wilayani Tarime, Gerald Ng’ong’a amesema ataanza kuwalipa mshahara wenyeviti wote wa vitongoji 26 vya kata hiyo.

“Nitaanza kuwalipa wenyeviti wa vitongoji wa kata ya Rabour kila mwezi,” Ng’ong’a ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya aliimbia Mara Online News kwa simu jana.

Alisema wenyeviti 26 wote wa kata hiyo wataanza kupokea mshahara wakati wowote kuanzia sasa.

Ng’ong’a ambaye ni maarufu kwa jina la GSN alisema ameamua kufanya hivyo ili kuwezesha wenyeviti hao kuwa na ari ya kushirikiana na wananchi na viongozi wengine kuharakisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika kata hiyo.

Aidha, Diwani huyo kupitia chama tawala - CCM alisema pia amegawa msaada wa vifaa vya ofisi kwa wenyeviti hao.

Rabour ni moja ya kata zinazotajwa kupiga hatua ya maendeleo ya kjamii katika wilaya ya Rorya, mkoani Mara katika miaka ya hivi karibuni.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages