NEWS

Friday, 31 January 2025

Mara: HAIPPA PLC yapokea wanahisa wapya, yanadi huduma zake



Sehemu ya wajumbe na wageni waalikwa wakifuatilia mada katika Mkutano Mkuu Maalum wa HAIPPA PLC mjini Musoma, Mara jana Januari 30, 2025.
--------------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Musoma

Kampuni ya HAIPPA PLC imepokea wanachama (wanahisa) wake wapya kadhaa katika Mkutano Mkuu Maalum uliofanyika mjini Musoma, mkoani Mara jana Januari 30, 2025.

Mkutano huo ulihudhuriwa na watu zaidi ya 300, wakiwemo wenyeviti na maofisa watendaji wa mitaa na kata, wajasiriamali, wanafunzi, wakulima na watu wenye ulemavu.

Baadhi ya wanahisa wapya waliotambulishwa na kupokewa katika mkutano huo.
---------------------------------

Aidha, HAIPPA PLC ilitumia mkutano huo kutambulisha huduma zake kwa wadau mbalimbali.

“Kampuni ya HAIPPA PLC inaenda kuwa miongoni mwa makampuni makubwa ya umma kwa ajili ya kusaidia ukuaji wa shughuli za uwekezaji nchini Tanzania,” Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, CPA Boniface Ndengo alisema na kuongeza:

“HAIPPA imekuja kama shule ya kujenga makampuni mapya na imetoa fursa kwa wenyeviti wa mitaa kubuni miradi ya kiuwekezaji ambayo itatushirikisha sisi kwa faida na manufaa ya watu wa maeneo yao.”

Mgeni rasmi katika mkutano huo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi ambaye aliwakilishwa na Afisa Biashara wa mkoa huo, Gambales Timotheo.

“Mara ni kituo cha kibiashara cha Jumuiya ya Afrika Mashariki, mkoa wetu unapakana na boda tatu. Sisi wenye ardhi kubwa na rasilimali nyingi kuliko wengine hatujazitumia ipasavyo, hakikisheni HAIPPA inakuwa jicho la kutangaza fursa tulizo nazo,” alisema Gambales.

Mgeni rasmi katika mkutano huo, Gambales Timotheo (wa tatu kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa HAIPPA PLC, CPA Boniface Ndengo, miongoni mwa viongozi wengine. (Picha zote na Mara Online News)
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages