NEWS

Wednesday, 29 January 2025

Wasira kuanza ziara mkoani Mara leo



Stephen Masato Wasira


Na Mwandishi Wetu/ Mara Online News

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, leo Jumatatu anaanza ziara ya kikazi mkoani Mara.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Idara ya Uenezi ya CCM Mara, Wasira atatembelea wilaya zote sita za mkoa huo, akianzia wilaya ya Bunda.

Hiyo itakuwa ziara yake ya kwanza mkoani Mara tangu achaguliwe na Mkutano Mkuu wa CCM Taifa hapo Januari 18, 2025 kushika madaraka hayo.

Wasira ni mmoja wa wanasiasa mashuhuri tangu enzi za kudai uhuru wa Tanganyika miaka ya 1950.

Amewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini tangu awamu ya kwanza ya uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere.

Baada ya kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Wasira alisema jukumu lake kubwa litakuwa kuimarisha chama hicho tawala ili kiendelee kushika dola.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages