
Tundu Antipas Lissu na
Freeman Aikael Mbowe
Tundu Antipas Lissu ametangazwa kuwa Mwenyekiti mpya wa CHADEMA Taifa baada ya kuvuna kura 513, na kumshinda Freeman Aikael Mbowe aliyepata kura 482 katika uchaguzi uliofanyika usiku wa kuamkia leo Jumatano.
Naye John Heche ameshinda nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Bara baada ya kupata kura 577 dhidi ya Ezekia Wenje (kura 372).
Matokeo hayo yametangazwa na mmoja wa wasimamizi wa uchaguzi huo wa kihistoria, Prof Raymond Mosha katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam muda mfupi uliopita leo Januari 22, 2025.
No comments:
Post a Comment