
Na Godfrey Marwa, Serengeti
Taasisi ya Nyansaho (NF) yenye makao makuu yake wilayani Serengeti, Mara wiki iliyopita ilishiriki katika mapokezi ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi wilayani humo kwa ziara ya ukaguzi wa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho tawala ya mwaka 2020-2025.
Mjumbe wa Nyansaho Foundation, Mtiro Kitigani, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa taasisi hiyo alisema ugeni huo ni fahari kwa wananchi wa Serengeti.

Mjumbe wa Nyansaho Foundation, Mtiro Kitigani, akizungumza wakati wa mapokezi hayo.
---------------------------------------
"Sisi kama Nyansaho Foundation tumeuopokea ujio wa Dkt Nchimbi kwa mikono miwili na ni fahari kubwa kwa wananchi wa Serengeti.
"Tunamshukuru Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara na Mkuu wa Mkoa wetu kutambua uwepo wetu, juhudi zetu zinaoneka hapa Serengeti na mko wa Mara kwa ujumla.
"Taasisi hii inajishughulisha kusapoti masuala ya elimu, afya na kwa wenye mahitaji wasiojiweza ndani na nje ya Serengeti," alisema Mtiro.
Alisema lengo la Nyansaho Foundation ni kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt Samia Suuhu Hassan katika kuwaleta wananchi maendeleo kwenye masuala ya afya, elimu na mahitaji maalum kwa wasiojiweza.
UNAWEZA PIA KUSOMA:
»Tarime: Shilingi zaidi ya milioni 48 zapatikana harambee ya kukamilisha ujenzi wa Kanisa la SDA Mtahuru
»Rorya wamshukuru Katibu Mkuu CCM Balozi Dkt Nchimbi kwa kukazia ujenzi wa barabara ya Utegi - Shirati - Kirongwe kwa lami
»MAKALA:Ujio wa CMG Hotels Ltd utakavyochochea ukuaji wa utalii, uchumi Tarime
»Waziri Kikwete aipongeza Barrick kwa matumizi ya teknolojia zenye usalama migodini
No comments:
Post a Comment