
Na Mwandishi Wetu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan, amewatakia Wakristo kheri ya Sikukuu ya Pasaka, na kusisitiza umuhimu wa kudumisha upendo, umoja na amani nchini.
“Nawatakia nyote kheri ya Sikukuu ya Pasaka ambapo ndugu zetu Wakristo wanaadhimisha kumbukizi ya kufufuka kwa Yesu Kristo,” Rais Samia ameandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii leo Jumapili Aprili 20, 2025.
“Siku hii njema ikawe pia ya tafakari kwetu sote juu ya upendo wetu kwa Muumba wetu na wenzetu juu ya kujitoa kwa bidii na weledi katika utekelezaji wa majukumu yetu popote pale tulipo juu ya kuendelea kujenga jamii inayoishi katika kweli na juu ya haki ambazo daima huambatana na wajibu kwetu sote.
“Kwa Pamoja tuendelee kuliombea Taifa letu kheri huku tukiishi na kutenda yale yanayowezesha nchi yetu kuendelea kubaki kuwa moja, imara, yenye amani na utulivu,” amesema Rais Samia.
Sikukuu ya Pasaka huadhimishwa na Wakristo duniani kote kama kumbukizi ya ufufuko wa Yesu Kristo, tukio linalobeba ujumbe wa matumaini, msamaha na uzima mpya.
No comments:
Post a Comment